BASTOLA ZILIZOKAMATWA.
Awali majambazi hayo yalivamia bar moja eneo la kilimahewa na kuwalaza watu chini kisha kupora mali zao na kuiba bastola ya mteja mmoja. Majambazi hayo yaliyokuwa katika gari dogo yalipostukia kuwa yanafuatiliwa yalianza kufyatua risasi hovyo hali iliyosababisha shughuli za biashara kwenye eneo la tukio kusimama kwa muda.
RISASI 14.Raia wema ndiyo waliofanikisha kukamatwa kwa majambazi hao kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ambao nao bila ajizi walifuatilia nyendo za majambazi hao na hatimaye kufanikiwa kuwatia nguvuni.Wawili kati ya majambazi hayo manne hali zao ni mbaya na wamepelekwa hospitali ya Rufaa Bugando, mmoja katwangwa risasi mguuni na takoni ile hali mwingine sugu anayetambulika kwa jina maarufu 'Askofu' akiwa amevunjika mguu kabisa kwa kutwangwa risasi wakati alipojaribu kuitoroka mikono ya polisi.
Jeshi la polisi mwanza linaendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya tukio zima ambamba na kuwahoji watuhumiwa wote wanne wa mkasa huo.
No comments:
Post a Comment