Wednesday, April 20, 2011

MAJAMBAZI YAKAMATWA JIJINI MWANZA

 Jana majira ya saa kumi na dakika kadhaa jioni jeshi la polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kuwatia nguvuni watu wanne wanaotuhumiwa kwa kufanya ujambazi wakiwa na bunduki moja aina ya smg na bastola mbili moja ikiwa na risasi 12 na na ya pili ikiwa na risasi 2. Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la polisi Mwanza Simon Sirro amesema kuwa watu hao wamekematwa katika eneo la mtaa wa libert jirani na benki ya NMB wakiwa kwenye harakati za safari kuelekea Nyegezi ambako walipanga kwenda kufanya uvamizi kwenye duka moja.
 BASTOLA ZILIZOKAMATWA.
Awali majambazi hayo yalivamia bar moja eneo la kilimahewa na kuwalaza watu chini kisha kupora mali zao na kuiba bastola ya mteja mmoja. Majambazi hayo yaliyokuwa katika gari dogo yalipostukia kuwa yanafuatiliwa yalianza kufyatua risasi hovyo hali iliyosababisha shughuli za biashara kwenye eneo la tukio kusimama kwa muda.
 RISASI 14.
Raia wema ndiyo waliofanikisha kukamatwa kwa majambazi hao kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ambao nao bila ajizi walifuatilia nyendo za majambazi hao na hatimaye kufanikiwa kuwatia nguvuni.Wawili kati ya majambazi hayo manne hali zao ni mbaya na wamepelekwa hospitali ya Rufaa Bugando, mmoja katwangwa risasi mguuni na takoni ile hali mwingine sugu anayetambulika kwa jina maarufu 'Askofu' akiwa amevunjika mguu kabisa kwa kutwangwa risasi wakati alipojaribu kuitoroka mikono ya polisi.

Jeshi la polisi mwanza linaendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya tukio zima ambamba na kuwahoji watuhumiwa wote wanne wa mkasa huo.

Saturday, April 16, 2011

Leo ni HEPI BESIDEI YANGU!!!

                                                      Thanks all !!!!! Karibu kwa pilau

Monday, April 11, 2011

Safu ya CCM hii hapa! Lowasa, Chenge, Rostam hawamo! Tafsiri yake nini?

Katibu Mkuu- Wilson Mukama
Naibu Katibu Mkuu (Bara) John Chiligati
Naibu Katibu Mkuu (Visiwani) -Vuai Ali Vuai
Katibu Mwenezi- Nape Nauye
Mambo ya Nje –Januari Makamba
Organaizesheni – Asha Abdala Juma
Uchumi na Fedha -Mwigulu Nchemba

WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU
Anna Abdalah
Peter Kisumo
Mwigulu Nchemba
Januari Makamba
Aly Juma Shamhuna
Wilson Mukama
Emmanuel Nchimbi.

WANAOINGIA KAMATI KUU
Pindi Chana
Abdulrahman Kinana
Zakhia Hamdan Meghji
Abdalah Kigoda
Steven Wasira
Costansia Buhiye
William Lukuvi
Dk. Hussein Ali Mwinyi
Dk. Maua Daftari
Samia Suluhu
Shanmsi Vuai Nahodha
Omary Yusuf Mzee
Prof. Makame Mbarawa
Mohamed Seif Khatibu

Monday, April 4, 2011

UNA MIAKA 30??? OMBA UONGOZI BARAZA LA VIJANA CHADEMA(BAVICHA)

Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, John Mnyika

Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Bavicha) ngazi ya taifa, linatarajia kufanya uchaguzi mwezi ujao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya chama hicho, John Mnyika, nafasi zitakazogombewa ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji, Mweka Hazina, Wawakilishi wa Bavicha kwenye Mkutano Mkuu wa chama na wawakilishi wa Bavicha kwenye Baraza Kuu la chama.

Alitaja umri unaoruhusiwa kugombea kwa mujibu wa Katiba umri wa ujana ni kati ya Miaka 18 na 35.

Alisema mgombea anatakiwa kugombea kwenye umri unaomruhusu kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa bado na umri wa Ujana; hivyo wagombea wenye umri wa zaidi ya miaka 30 hawataruhusiwa kugombea ili kufanya viongozi wa vijana wasiwe zaidi ya miaka 35 katika kipindi chao chote cha utumishi katika Bavicha.

" Wagombea watachukua na Kurudisha Fomu kuanzia tarehe 4 Aprili hadi tarehe 26 Aprili. Fomu zitatolewa kuanzia ngazi ya Mkoa, Makao Makuu ya chama," alisema Mnyika.

Alisema kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watalipia shilingi elfu thelathini.

Alisema waliogombea uchaguzi wa awali uliofutwa watajaza na kulipia upya hata kama waliogombea nafasi hizo hizo wanazogombea sasa kwa mujibu wa kanuni za chama.

Alisema mikutano ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wawakilishi wa Bavicha kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Bavicha kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu.

Alisema Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watapendekezwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha na uteuzi wao utathibitishwa na Kamati Kuu ya chama.

Kuhusu kampeni, Mnyika alisema kampeni za uchaguzi zitafanywa kwa kuzingatia kanuni za chama, maadili ya uongozi/viongozi pamoja na muongozo juu ya uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama uliopitishwa na Baraza Kuu la Chama unafafanua mambo yanayopaswa kufanywa na yasiyopaswa kufanywa wakati wa kampeni na uchaguzi ndani ya chama kwa lengo la kujenga mshikamano na umoja ndani ya chama na kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki.